REVOLUTIONARY GOVERNMENT OF ZANZIBAR | Civil Service Commission
Africa/Dar_es_Salaam (EAT)

Sera ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (Privacy Policy)

Tume ya Utumishi Serikalini inatambua umuhimu wa kulinda taarifa binafsi za wananchi wote wanaotumia mfumo huu, kwa kuzingatia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 (Personal Data Protection Act, 2022).

1. Ukusanyaji wa Taarifa

Tunakusanya taarifa zinazohitajika kisheria kwa ajili ya mchakato wa ajira pekee, ikiwa ni pamoja na: Majina kamili, Namba ya NIDA, Tarehe ya Kuzaliwa, Vyeti vya Elimu, Uzoefu wa kazi, na Mawasiliano.

2. Uhifadhi na Usalama

Vyeti na nyaraka zote za wananchi zimehifadhiwa kwenye seva salama ya Serikali (Protected Storage) na haziwezi kutazamwa na umma wala mtu yeyote asiyehusika na mchakato wa mchujo wa nafasi uliyoiomba.

3. Haki za Mwombaji

Una haki ya kutazama taarifa zako, kuzisahihisha, na kupata nakala ya wasifu wako muda wowote.